Umoja wa Mataifa?wasema mapigano nchini Sudan yanavuruga utaratibu wa biashara

(CRI Online) Oktoba 24, 2023

Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema, athari za kuvuka mpaka za mapigano yanayoendelea nchini Sudan zimeathiri sana biashara kati ya nchi hiyo na Sudan Kusini, na pia kuongeza idadi ya raia wa Sudan Kusini wanaorejea nchini humo kutoka Sudan.

OCHA imesema mapigano hayo kati ya Jeshi la Sudan na Kikosi cha Mwitikio wa Haraka (RSF) yaliyoanza katikati ya Mwezi April mwaka huu, yamepunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje, na hivyo kusababisha kupanda kwa bei za vyakula nchini Sudan Kusini.

Pia Ofisi hiyo imeripoti kuwa, watu 317,993 wameingia nchini Sudan Kusini kutoka Sudan tangu kuanza kwa mapigano hayo, na kuongeza kuwa, nusu ya watu hao ni wanawake, na nusu ya watoto ni wenye umri wa chini ya miaka 18.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

又大又粗又爽又黄的少妇_国产欧美日韩亚洲精品区_欧美重口另类在线播放二区_边做饭边被躁在线播放