

Lugha Nyingine
Mkutano wa UN?watoa wito wa kuzidi kushughulikia habari katika tume za kulinda amani
Mkutano wa maandalizi kwa ajili ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 2023 umefanyika Jumatatu mjini Kigali nchini Rwanda, ambapo washiriki wamesisitiza umuhimu wa kuimarisha mbinu za kukabiliana na changamoto za habari zilizomo ndani ya tume za kulinda amani.
Kwenye mkutano huo, Waziri wa Ulinzi wa Rwanda Bw. Juvenal Marizamunda amesisitiza umuhimu wa mkutano huo, kwa kuwa tume za kulinda amani kote duniani zinakabiliwa na changamoto kwenye kazi za usambazaji askari. Amesema changamoto hizo zinaathiri zaidi kazi kuu ya kuwalinda raia ambapo habari potofu, za uongo na kauli za chuki zinaenea kwa kasi zaidi kupitia vyombo vya habari vya kijamii.
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UN anayeshughulikia mambo ya Afrika Martha Ama Akyaa Pobee ametoa wito wa kuweka mkakati wa mawasiliano wa pande zote unaoendana na masuala makuu ya kisiasa na kiusalama.
Kutalii Hifadhi ya Taifa ya Nairobi nchini Kenya kupitia lenzi ya kamera
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
Katika Picha: Mandhari ya magenge kwenye Mto Manjano huko Henan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma