

Lugha Nyingine
Mwanadiplomasia mwandamizi wa China atoa wito wa kuzuia mapigano kati ya Palestina na Israel yasizidi kuongezeka
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema ni muhimu kuzuia hali ya kuchochea na kusababisha matatizo makubwa zaidi ya kibinadamu katika mapigano yanayoendelea kati ya Palestina na Israel.
Waziri Wang ameyasema hayo siku ya Jumatatu alipoongea kwa simu na mwenzake wa Israel Eli Cohen, ambapo Cohen ameeleza msimamo wa Israel na wasiwasi wake wa kiusalama kuhusu mgogoro kati ya Palestina na Israel.
Bw. Wang amebainisha kuwa China ina wasiwasi mkubwa juu ya kuendelea kwa hali ya kuchochea vita na athari zinazozidi kuwa mbaya, na kusikitishwa sana na idadi kubwa ya vifo vya raia vilivyosababishwa na vita.
Amesema China inalaani vitendo vyote vinavyodhuru raia na kupinga ukiukaji wowote wa sheria ya kimataifa, na kuongeza kuwa nchi zote zina haki ya kujilinda, lakini zinapaswa kuheshimu sheria ya kimataifa ya kibinadamu na kulinda usalama wa raia. Hivyo amesema maafikiano ya jumuiya ya kimataifa ni kuwepo kwa suluhu ya nchi mbili.
Wakati huohuo Bw. Wang amefanya mawasiliano kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Riyad Al–Maliki ambapo amefafanua kuwa kinachohitajika zaidi katika Ukanda wa Gaza ni juhudi za kuleta amani, usalama, chakula na dawa, badala ya vita, silaha na risasi ama hesabu za siasa za kijiografia.
Kutalii Hifadhi ya Taifa ya Nairobi nchini Kenya kupitia lenzi ya kamera
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
Katika Picha: Mandhari ya magenge kwenye Mto Manjano huko Henan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma