

Lugha Nyingine
Wataalamu na maafisa watoa wito wa kuongezwa ushirikiano kati ya China na Ethiopia katika TVET
ADDIS ABABA - Wataalamu na watunga sera waliohudhuria semina ya ngazi ya juu kuhusu ushirikiano wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) kati ya China na Afrika wametoa wito wa kuimarisha uhusiano kati ya China na Ethiopia katika elimu ya TVET.
Semina ya Ushirikiano na Mabadilishano kitaaluma kuhusu TVET kati ya China na Afrika iliyofanyika Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, siku ya Jumapili iliwakutanisha maafisa waandamizi wa serikali ya Ethiopia, maafisa wa China, wasomi na wataalam, miongoni mwa wengine.
Kwenye semina hiyo, Teshale Berecha, Waziri wa Kazi na Ustadi wa Ethiopia, amesisitiza haja muhimu ya kuhimiza kufundishana na kushirikiana kwa pamoja kati ya Ethiopia na China katika nyanja ya TVET.
"Ushirikiano katika elimu ya TVET siyo tu ni jitihada za kitaaluma; ni daraja linalounganisha nchi zetu, kuongeza uelewa wa pamoja, na kuimarisha uhusiano unaotuunganisha pamoja," Berecha amesema.
Amesema Wizara ya Kazi na Ustadi ya Ethiopia "inasimama kama nguvu inayosukuma azimio letu la pamoja la kuimarisha ushirikiano katika nyanja ya TVET kati ya Ethiopia na China."
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Muungano wa Elimu ya Ufundi wa China na Afrika, Gong Zhiwu, amesema muungano huo umezindua miradi katika nchi kadhaa za Afrika, zikiwemo Ethiopia, Tanzania, Rwanda, Kenya, Uganda na Ushelisheli.
“Nchini Ethiopia, muungano umekuwa ukifanya kazi kwa karibu sana na Wizara ya Kazi na Ustadi ya Ethiopia juu ya mapitio ya pande zote na uboreshaji wa mfumo wa TVET nchini, ikiwa ni pamoja na sera na miongozo ya TVET, viwango vya kazi, mtaala, zana za tathmini, na ujenzi wa uwezo wa wafanyakazi na kitivo, uhusiano wa viwanda,” amesema Gong, huku akifafanua juu ya ushirikiano huo unaohusisha maeneo ya maendeleo ya viwanda, miundombinu ya kiuchumi, madini na uchimbaji, afya, kilimo, biashara, utamaduni wa michezo na utalii.
Kutalii Hifadhi ya Taifa ya Nairobi nchini Kenya kupitia lenzi ya kamera
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
Katika Picha: Mandhari ya magenge kwenye Mto Manjano huko Henan, China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma