Makumi ya maelfu ya Waalgeria waandamana kulaani mashambulizi ya Israel dhidi ya?Gaza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 20, 2023
Makumi ya maelfu ya Waalgeria waandamana kulaani mashambulizi ya Israel dhidi ya?Gaza
Watu wakishiriki katika maandamano ya kuonyesha hisia zao za kuunga mkono Wapalestina huko Algiers, Algeria, Oktoba 19, 2023. (Xinhua)

Algiers - Makumi kwa maelfu ya Waalgeria wameingia mitaani siku ya Alhamisi ili kuonyesha mshikamano wao na Wapalestina na kulaani mashambulizi ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

Katika mji mkuu, Algiers, umati wa watu umeandamana katika mitaa mikubwa kabla ya kuketi katika Eneo la Mashujaa waliojitoa mhanga, matangazo ya moja kwa moja ya Shirika la Utangazai la Serikali, ENTV yameonyesha.

Huku wakipeperusha bendera za Palestina na Algeria, waandamanaji hao walitamka kwa shauku kauli mbiu zinazoiunga mkono Gaza, wakitaka haki itendeke kwa maisha ya watu yaliyopotea, na kutaka kukomeshwa kwa ukatili wa Israel dhidi ya raia.

Waandamanaji hao walikuwa wanadai Palestina iwe huru na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati mara moja.

Wametoa wito kwa viongozi wa nchi mbalimbali duniani kuishinikiza Israel kuondoa vikwazo dhidi ya Gaza na kusitisha mashambulizi yake katika eneo la Palestina, wakisisitiza haja ya haraka ya kufungua vivuko vya mpaka na kupeleka misaada na vifaa tiba kwa watu wa Gaza.

Kwa mujibu wa ENTV, maandamano pia yamefanyika katika majimbo mengine ya Algeria.

Oktoba 7, Vuguvugu ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilianzisha mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya maeneo ya kijeshi ya Israel na miji iliyo karibu na Ukanda wa Gaza, na kusababisha mashambulizi makubwa ya anga ya Israel dhidi ya Gaza na hatua nyingine za adhabu, ikiwa ni pamoja na kudhibitiwa kwa eneo hilo huku usambazaji wa maji, umeme, mafuta na mahitaji mengine ukikoma.

Takriban watu 1,300 nchini Israel wameshauawa katika mashambulizi yaliyoanzishwa na Hamas. Wakati huo huo, Wizara ya Afya yenye makao yake makuu mjini Gaza imesema idadi ya Wapalestina waliofariki kutokana na mashambulizi ya Israel huko Gaza imefikia 3,478.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha

又大又粗又爽又黄的少妇_国产欧美日韩亚洲精品区_欧美重口另类在线播放二区_边做饭边被躁在线播放