Wageni kutoka nchi mbalimbali watembelea Yan’an na kuhisi moyo wa mapinduzi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2023
Wageni kutoka nchi mbalimbali watembelea Yan’an na kuhisi moyo wa mapinduzi
Ujumbe wa “Kuongeza Mawasiliano na Maelewano kati ya Watu” wa wageni wa nchi mbalimbali ukitembelea kwenye Jumba la Makumbusho la Historia ya Kijiji cha Liangjiahe. (Picha ilipigwa na Zhou Yu/People’s Daily Online)

Tarehe 9, Oktoba, ujumbe wa wageni kutoka nchi mbalimbali ulioalikwa na Mfuko wa Maendeleo ya Amani wa China ulikwenda kwenye Kijiji cha Liangjiahe cha Mji wa Yan’an, Mkoa wa Shaanxi, China kutembelea jumba la makumbusho la historia ya kijiji hicho na sehemu nyingine, ambapo kwa kupitia maelezo ya hapo hapo, walifahamishwa zaidi hadithi kuhusu moyo wa mapinduzi wa China.

Martin Azzorpardi ni mwalimu wa “Kona ya China” ya Shule ya Sekondari ya St. Margaret's nchini Malta. Aliwahi kuja China kutembelea mara nyingi na kuwa na upendo mkubwa kwa China. “Malta ni moja ya nchi zilizoshiriki kwanza kwenye pendekezo la kujenga pamoja ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’, naona fahari kwamba nchi yangu kuwa mshiriki wa pendekezo hilo. Pendekezo hilo linaunganisha tamaduni mbalimbali, na kuhimiza mshikamano wa watu wa nchi mbalimbali, hali ambayo ndiyo tunayoihitaji. Hatutaki vita, tunapenda kunufaishana kutokana na utamaduni wa aina mbalimbali na kubadilishana maoni yetu.” Alipomaliza kusema aliimba wimbo wa jadi wa China “Maua ya Jasmine”.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu wa Tanzania Bw. Nawanda alisema safari hiyo ni yenye thamani kubwa. “Safari hiyo ya kutembelea Yan’an inaniwezesha kuijua China zaidi. China ni nchi inayofuata shirikishi, sisi Watanzania tunanufaika na hiyo pia” alisema Nawanda.

Tarehe 10, Oktoba, ujumbe huo umetembelea Jumba la Makumbusho ya Mapinduzi la Yan’an, na Eneo la Mabaki ya kituo cha Mapinduzi cha Yangjialing. Zoon Ahmed, mtafiti wa Jumuiya ya washauri mabingwa ya utandawazi wa uchumi duniani alikuwa amepata mengi baada ya kutembelea Eneo la Mabaki ya kituo cha Mapinduzi cha Yangjialing, na alimwambia mwandishi wa habari kuwa, “wanachama wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) wa kizazi hadi kizazi wana moyo wa kubeba jukumu na kutimiza malengo, hawa ni jiwe la msingi wa kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. Kujitolea kwao bila ya ubinafsi kunastahiki kusifiwa.” Aliongeza kuwa, “darasa la historia” linalowavutia watu kama hilo siyo tu linawawezesha vijana waelewe zaidi nchi yao, bali pia linawasaidia watu wa nchi nyingine kuijua zaidi na kuielewa zaidi China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha

又大又粗又爽又黄的少妇_国产欧美日韩亚洲精品区_欧美重口另类在线播放二区_边做饭边被躁在线播放