

Lugha Nyingine
Changchun:? "Mji wa magari" unaokumbatia siku za baadaye
Ukiingia katika Mji wa Changchun ulioko Mkoa wa Jilin wa China, unaweza kuona magari ya chapa ya "Hongqi" na "Jiefang" yakipita mitaani kila mahali. Njia za reli za tramu zenye historia ndefu huchanganyika katika mkondo usio na mwisho wa watu na kuwa sehemu isiyoweza kutenganishwa ya maisha ya kila siku ya raia.
Treni ya umeme ya mwendokasi ya Fuxing huunganisha sehemu mbalimbali za China kutoka hapa, na magari ya chapa ya "Hongqi" yanaendeshwa kutoka hapa hadi Mashariki ya Kati na Ulaya... Hapa ndipo lilipo chimbuko la viwanda vya magari na usafiri wa reli wa Jamhuri ya Watu wa China, ambapo gari la kwanza na kizazi cha kwanza cha treni za chini ya ardhi (subway) nchini humu vilizaliwa. Leo, mji huo unatumia vizuri rasilimali zake tajiri za viwanda vya magari na uwezo mkubwa wa uvumbuzi wa kiteknolojia kuhimiza maendeleo na kuwa kimataifa zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma